Latest Posts

KATIBU TAWALA MORO: TUMEANZA KUJINOA KWAAJILI YA SHIMIWI

Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wametakiwa kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi huku akiwataka kutumia vema mazingira mazuri ya Ofisi hiyo katika kufanya mazoezi kwa lengo la kuiweka timamu miili yao nakuepusha magonjwa madogomadogo yanayoweza kuepukika.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro   Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Alhaji Dkt. Mussa Ali Mussa wakati akizindua rasmi klabu ya mazoezi ya Ofisi hiyo iliyofanyika eneo la maporomoko ya Maji ya CHOMA yaliyopo nje kidogo na Ofisi hiyo.

Amesema, Ofisi yake imefikia uamuzi wa kuanzisha Club hiyo inayojulikana kwa jina la “RAS MOROGORO JOGGING CLUB” ili kuimarisha Afya za watumishi wake nakutekeleza agizo la Serikali la kila Ofisi ya Umma iwe naprogram ya watumishi wake kufanya mazoezi ili kulinda afya za watumishi hao.

Aidha, amesema mazoezi hayo yatakuwa endelevu hukuakibainisha kuwa yatakwenda sambamba na kutembelea maeneoya utalii kama walivyotembelea maporomoko ya CHOMA ilikuyatangaza lakini pia kuyaboresha pale inapobidi kwakushirikiana na mamlaka zinazohusika.

Amesema, Ofisi yake itakuwa tayari kushirikiana na Viongozi wa Sekta mbalimbali na kupeleka mahitaji muhimu kama UMeme, Maji, Barabara na huduma za Afya ili kuhakikisha Maisha ya wanaozunguka vivutio hivyo yanaboreka nakunyanyua Maisha yao Pamoja na kuongeza thamani ya maeneohayo.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo amesema kuzinduliwa kwa klabu hiyo kunachocheo maandalizi yakwenda kupata ushindi wa kishindo kwenye mashindano yashirikisho la michezo ya wizara na idara za serikali (SHIMIWI) yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza kuanzia Septemba 1 hadi 16 mwaka huu.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Michezo Mkoa wa Morogoro Grace Njau amesema ili mazoezi ya watumishi kuwaendelevu imewekwa ratiba maalum ya siku tatu kwa wiki kuanzia saa 10:00 hadi saa 11:00 jioni watumishi wotewanaungana Pamoja kufanya mazoezi.

Naye Justine Mnyandwa kwa niaba ya watumishi wa Ofisi hiyo amesema kuwa kuna faida kubwa ya kufanya mazoezi hayo, amesema nje ya kuimarisha Afya za watumishi kwakuepuka magonjwa yasiyoambukiza bado mazoezi hayo yanadumisha Ushirikiano, Upendo na umoja miongoni mwa watumishi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!