Latest Posts

WAKULIMA 300 MOROGORO WANUFAIKA NA UWEPO WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI

Na Mwandishi Wetu

Zaidi ya wakulima 300 kutoka mkoa wa Morogoro wamenufaika na uwepo wa Kiwanda cha Sukari cha  Mkulazi ambacho kinanunua miwa yao kwa ajili ya uzalishaji wa sukari yenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Afisa Uhusiano wa Kiwanda hicho, Clementina Patrick, amesema  lengo la ushiriki wao katika maonesho hayo si tu kutambulisha bidhaa, bali ni kuwa karibu na wananchi kwa kuwapatia sukari  bora inayozalishwa kwa kutumia mitambo ya kisasa.

“Uwepo wa kiwanda hiki umeleta mabadiliko makubwa kwa jamii, wakazi  wa maeneo ya jirani, hususan wakulima wa miwa  wana uhakika wa soko la mazao yao  na hivyo kukuza uchumi wao,” amesema  Clementina.

Kwa mujibu wa  clementina, Kiwanda cha Mkulazi kinatoa sukari yenye ujazo tofauti tofauti kuanzia kilo  moja, kilo 25 na hadi kilo 50, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wananchi wa kipato cha aina yoyote,  wanapata bidhaa hiyo muhimu kwa matumizi ya nyumbani na matumizi mengine.

“Wananchi wanakaribishwa kutembelea banda letu Dodoma na Morogoro, tumeweka  bei rafiki kwa kila aina ya kipato kwa lengo la kuhakikisha kila mtu anapata sukari bora ” ameongeza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!