Hali ya taharuki ilitanda katika mtaa wa Itezi mjini Mbeya wiki iliyopita baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Miriam kuanza kugeuka kiviumbe cha ajabu ghafla. Kile kilichoanza kama maumivu ya miguu kiligeuka kuwa kisa cha kushtua kila mtu: miguu yake ilianza kubadilika na kuchukua umbo linalofanana na la mbuzi.Kwa mujibu wa mashuhuda, Miriam aliamka asubuhi akilalamika miguu kuwaka moto, na kabla ya jioni alikua hawezi tena kuvaa viatu. Ngozi ya miguu yake ilikuwa imekuwa nene, yenye nywele na kwato ndogo zilizoanza kujitokeza.
“Wakati tulimwona, tulifikiri ni mzaha ama maigizo,” alisema jirani yao Bi Zubeda. “Lakini tuliposogea karibu, tukashuhudia miguu yake imeshabadilika kweli, na alikuwa akilia kama mnyama.”
Watu walikusanyika kwa wingi kushuhudia tukio hilo. Familia yake ilibaki kinywa wazi, wakishindwa kuelewa kilichokuwa kikitokea kwa dada yao. Hata hivyo, mama yao aliyeonekana mwenye huzuni alisimama na kutoa siri nzito iliyopelekea hali hiyo. Soma zaidi hapa.