Na Theophilida Felician.
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala nchini wametakiwa kuwa makini na kuepuka kushiriki imani za kushirikina ili kuepukana na madhara yanaweza kusababishwa na imani hizo kwa jamii.
Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama cha waganga TAMESOT Bw Lukas Joseph Mlipu katika taarifa yake aliyoitoa baada yakuhitimisha maadhimisho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika yaliyokuwa yakifanyika mkoani Dodoma tangu Tarehe 25 na kuhitimishwa Tarehe 31 Agost mwaka huu wa 2025.
Katibu Lukas amesema maadhimisho hayo yamewakutanisha waganga kutoka mikoa mbalimbali ambapo dhamira ya kuwakutanisha pamoja ni kuwapa elimu stahiki yenye kuwaongezea ujuzi na maarifa katika utoaji huduma yatiba kwa wananchi, kuzingatia miongozo muhimu na misingi ya tiba asili kutoka baraza la tiba asili na tiba mbadala namengineyo mengi.
Amesema katika maadhimisho hayo zilitolewa nasaha mbalimbali kwa waganga zikiwataka kuyaepuka mambo yanayokwenda kinyume na miongozo ya taaluma ya tiba asili hasa ramuli chonganishi na imani za kishirikina  hususani kipindi hiki muhimu cha uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais kwani imani hizo zinaweza kuchochea hali ya uvunjifu wa amani kwa jamii husika.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa maadhimisho ya tiba asili ya mwafrika kwa mwaka huu haya kufanikiwa vizuri kutokana na uchache wa waganga waliojitokeza kushiriki akizibainisha baadhi ya sababu zilizopelekea hali hiyo ni mwamuko mdogo uliokuwepo kwa baadhi ya waratibu wa wabaraza la tiba asili mikoa na wilaya katika zoezi la kuwahamasisha ushiriki maadhimisho hayo.
Hata hivyo amewashukuru waganga wote waliojitokeza na kushiriki vyema tukio hilo mwaka huu ambapo amewasihi kuyazingatia yote waliyonufaika nayo kwenye matukio ya wiki hiyo huku akiishukuru serikali ilivyokuwa nao bega kwa bega hadi kukamilisha shughuli za wiki ya tiba asili ya mwafrika bila kuvisahau vyama vingine vya waganga vilivyoshirikiana na TAMESOT katika zoezi zima la tamasha.
Katibu mkuu huyo ambaye aliifikia mikoa 11 ya Tanzania bara alikuwa miongoni mwa wa jumbe 15 walioteuliwa kuwafikia waganga na kuwahamasisha juu ya kufahamu umuhimu wa wiki yatiba asili ya mwafrika kwa waganga nchini.