Latest Posts

MARIOO KUTUMBUIZA MKWAWA RALLY OF TANZANIA

Kuelekea katika ufunguzi wa Mashindano ya Mbio za Magari Barani Afrika – Mkwawa Rally of Tanzania, ambayo ni mzunguko wa mwisho wa African Rally Championship (ARC) baada ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, bingwa wa Afrika atapatikana rasmi kwenye Milima ya Uluguru mkoani Morogoro.

Katika shamra shamra za uzinduzi, msanii nyota wa kizazi kipya – Marioo atapiga burudani kali katika kiwanda cha Mkwawa, mahali ambapo kutafanyika ufunguzi wa mashindano hayo.

Mashabiki kutoka mataifa jirani ya Uganda, Kenya na Burundi wanatarajiwa kufika kushuhudia mashindano haya, na watakutana na vibe kali kutoka mashabiki wa Tanzania wanaokuja kutoka Arusha, Mbeya, Iringa, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam na pia Team ya Amapiano Motorsports.

Kwa upande wa ARC, Yassin Nasser na Samman Vohra wako katika pambano kubwa la kuwania taji la mwaka huu. Wakati huo huo, madereva wengine wanakuja kwa nguvu wakitaka kupangua nafasi tatu za juu.

Kwa upande wa Tanzania, huu utakuwa mzunguko wa nne wa National Rally Championship (NRC) kuelekea kumpata bingwa wa Taifa, huku mbio za mwisho zikitarajiwa kufanyika Novemba mkoani Arusha.

Bingwa mtetezi Manveer Birdi (Mitsubishi Evo 09) atakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa kaka yake Randeep Singh Mistubishi EVO 09), Gurpal Sandhu (Mitsubishi Evo 10), na Ahmed Huwel (Toyota Yaris R5) ambaye anawinda ubingwa kwa mara nyingine tena,Washindani wengine wanaoweza kuharibu mpangilio wa nafasi tatu bora ni,Shehzad Munge – Mitsubishi Evo X,Samir Nahdi Shanto – Ford Prota,Altafu Mungu – Ford Fiesta R5,Dharam Pandya – Subaru VAB

Kwa upande wa washiriki wa kimataifa, Hassan Alwi kutoka Uganda (Ford Proto) Akif Virani kutoka Kenya (Skoda Fabia) Mohammed Roshanali kutoka Burundi (Subaru Impreza NR4) watakuta na visiki vya watanzania Ahmed Farid Vigwaza (Ford Proto) Waleed Nahdi (Subaru Impreza NRC3)Prince Charles (Mistubishi EVO 09) Charles Bicco (Subaru NRC3) wameahidi kushindana vikali na kuleta burudani kwa Mashabiki wao.

Mashindano haya yanatarajiwa kuwa ya kipekee zaidi kwa mashabiki, hasa kwenye vitasa vya magari aina ya R5 ambapo kutakuwa na Toyota Yaris, Skoda Fabia na Ford Fiesta (jumla ya sita). Vilevile, Ford Proto tatu na Mitsubishi Evo X tatu zitaongeza mvuto wa mashindano haya.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!