Kampuni ya GN ECO SOLUTION COMPANY imefanikiwa kuandaa na kuratibu programu maalumu ya ujenzi wa timu (Team Building) kwa wafanyakazi wa National Board of Accountants and Auditors (NBAA), iliyofanyika katika mazingira ya asili na utulivu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Programu hiyo imefanyika siku ya Jumamosi ikihusisha mazoezi na michezo mbalimbali ya kiutendaji iliyolenga kuimarisha mshikamano kazini, kuendeleza mawasiliano bora, kujenga uaminifu baina ya wafanyakazi, pamoja na kukuza misingi ya uongozi na ushirikiano wa pamoja. Kupitia mbinu shirikishi na za vitendo, washiriki wamehamasishwa kufanya kazi kama timu moja, kushirikiana katika kutatua changamoto na kujifunza umuhimu wa kutegemeana katika kufanikisha malengo ya pamoja ya taasisi.
Picha zinaonesha wafanyakazi wa NBAA wakishiriki kwa ari na furaha katika shughuli mbalimbali za vikundi, wakionesha mshikamano, maelewano na hali ya kuaminiana, hali inayoakisi mafanikio ya programu hiyo katika kujenga mahusiano chanya kazini. Aidha, wawezeshaji kutoka GN ECO SOLUTION wameongoza shughuli hizo kwa weledi, wakitoa maelekezo, motisha na msukumo unaolenga kuboresha utendaji kazi wa washiriki wanaporejea katika majukumu yao ya kila siku.
GN ECO SOLUTION COMPANY imeeleza kufurahishwa na ushirikiano huo na NBAA, ikisisitiza kuwa itaendelea kutoa programu bunifu, zenye tija na matokeo chanya katika kujenga rasilimali watu, kuongeza morali ya kazi na kuimarisha ufanisi wa taasisi za umma na binafsi nchini.
