Latest Posts

IRAN YALIPIZA KISASI NDANI YA ISRAEL; TRUMP ATISHIA KUINGIZA JESHI LA ARDHINI NA “KUFUTA” MIUNDOMBINU YA IRAN

Hali ya usalama duniani imetikisika leo asubuhi baada ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la Iran (IRGC) kurusha makombora mazito katikati mwa Israel, huku mataifa makubwa yakijiandaa kwa vita vya muda mrefu. Shambulio hilo la kulipiza kisasi limeua watu wawili mjini Ramat Gan, karibu na Tel Aviv, ikiwa ni jibu la kuuawa kwa mkuu wa usalama wa Iran, Ali Larijani, na kamanda wa Basij, Gholamreza Soleimani.

Wakati moshi ukifuka nchini Israel, nchini Lebanon, mashambulizi ya kushtukiza ya anga ya Israel jijini Beirut yameua watu sita na kujeruhi wengine 24 leo asubuhi, huku majengo yanayodaiwa kutumiwa na Hezbollah yakiteketezwa.

Katika hatua ya kushangaza, Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi Marekani (NCTC), Joe Kent, amejiuzulu leo akipinga ushiriki wa Marekani katika vita hivyo. Kent amedai kuwa Marekani imeingia vitani kutokana na shinikizo la Israel na si kwa sababu ya tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Marekani. Rais Trump amejibu kujiuzulu huko kwa kumwita Kent kuwa ni kiongozi “dhaifu” kwenye masuala ya usalama.

Akizungumza kutoka Oval Office, Rais Trump amesisitiza kuwa Marekani haina mpango wa kuondoka Iran hivi karibuni na yuko tayari kupeleka wanajeshi wa ardhini (Ground Troops).

“Tukiondoka sasa, itawachukua miaka 10 kujenga upya kile tulichoharibu. Hatuko tayari kuondoka bado,” amesema Trump, huku akionesha nia ya kushambulia vyanzo vya nyuklia na kisiwa cha nje cha mafuta cha Kharg Island nchini Iran.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!