Latest Posts

JIBU KWA MAREKANI? KOREA KASKAZINI YAONESHA VIFARU VINAVYOWEZA KUDAKA DRONES NA MAKOMBORA ANGANI.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesimamia zoezi kubwa la kijeshi lililolenga kuonesha uwezo wa kifaru kipya cha kivita, ambacho amekitaja kuwa ni silaha yenye ulinzi madhubuti na ya kipekee duniani.

Zoezi hilo lilifanyika jana Alhamisi katika Kambi ya Mafunzo ya Pyongyang Na. 60, ambapo vikosi vya vifaru vilionesha uwezo wa kushambulia kwa makombora ya anti-tank, huku vikosi vya nyuma vikiharibu ndege zisizo na rubani (Drones) na helikopta za adui zilizokuwa zimeigizwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali (KCNA), kifaru hicho kimeundwa kwa teknolojia ya hali ya juu inayokifanya kiwe na uwezo mkubwa wa kutambua na kuzuia mashambulizi ya makombora na drones kabla hayajakigusa.

“Nimefurahi sana kuona vifaru hivi vikisonga mbele kwa kishindo na kuitikisa ardhi. Tumepiga hatua kubwa katika kisasa sekta ya utengenezaji vifaru. Nina uhakika hakuna silaha ya kivita yenye ulinzi imara kama kifaru hiki duniani kote,” amesema Kim Jong Un kwa kuridhika.

Mazoezi haya yamekuja wakati kukiwa na mivutano mikubwa katika rasi ya Korea, kufuatia mfululizo wa majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini na mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya “Springtime” yaliyomalizika hivi karibuni kati ya Marekani na Korea Kusini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!