Latest Posts

“MSIITE KUSHINDWA KWENU KUWA NI ‘MAKUBALIANO”, JESHI LA IRAN LAMCHANA TRUMP

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) kupitia Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya, limeonekana kuzima matumaini ya amani yaliyotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump, likisema kuwa madai ya kuwepo kwa mazungumzo ni propaganda za kujidanganya na kwamba Marekani “imeingia kwenye mtego” usio na njia ya kutokea.

Msemaji wa makao makuu hayo Ebrahim Zolfaghari, amesisitiza kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na kwamba Iran haitakaa meza moja na mtu kama Trump. Zolfaghari ameenda mbali zaidi na kuonya kuwa dunia isitegemee kuona bei ya mafuta ikirejea katika hali ya zamani mpaka pale Marekani itakapofuta wazo la kuishambulia Iran.

Zolfaghari amesema kuwa Marekani inajaribu kupaka rangi “ushindi wa kimkakati” wa Iran kwa kuuita ni “mazungumzo.”

“Nguvu ya kimkakati mliyokuwa mkiisifia imegeuka kuwa ushindi wa kimkakati kwetu na kushindwa kwenu. Kama huyo anayejiita ‘mwenye nguvu duniani’ angekuwa na uwezo wa kujinasua katika mtego huu, angekuwa ameshafanya hivyo hadi sasa. Msiite kushindwa kwenu kuwa ni ‘makubaliano’. Enzi za ahadi zenu zimefikia kikomo”, amesema Zolfaghari.

Msemaji huyo ameweka wazi kuwa utulivu wa soko la nishati duniani sasa uko mikononi mwa majeshi ya Iran. Amesema bei ya mafuta na nishati haitashuka, na uwekezaji wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati hautakuwa na usalama mpaka pale utashi wa Iran utakaporidhika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!