Latest Posts

SANGU AAGIZA OSHA KUCHUKUA HATUA MIGODINI ‎

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu ameagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) kuendelea kutoa elimu kwa wamiliki wa migodi na wachimbaji kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama na afya mahala pa kazi, ili kulinda maisha ya wafanyakazi na kuongeza tija katika sekta ya madini.

‎Agizo hilo amelitoa Agosti 4, 2026, alipotembelea migodi ya Lindi Graphite Technologies Ltd na Elianje Genesis Ltd (Namungo) wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, kwa lengo la kukagua uzingatiaji wa sheria za usalama na afya mahala pa kazi.

‎Waziri Sangu amesema serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha usalama na afya ya Watanzania wanaofanya kazi katika migodi ya dhahabu na graphite vinaimarishwa, huku wachimbaji wakifanya kazi katika mazingira salama na yenye staha.

‎Amesema serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya kazi ili wachimbaji wadogo na wafanyakazi wote wa migodini waweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa bila kuhatarisha afya na usalama wao.

‎Aidha, amesema serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050, ikiwa ni pamoja na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa na kuzalisha ajira nyingi kwa Watanzania.

‎Kwa upande wake, Afisa Utumishi wa Lindi Graphite Technologies Ltd, Clement Mvuma, amesema kampuni hiyo imetoa ajira 230 kwa Watanzania na 15 kwa wataalamu wa kigeni, huku ikiwa imeanza kuzalisha tani 2,000 za graphite kwa wastani wa tani 70 hadi 80 kwa siku.

‎Naye Katibu wa Wachimbaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Elianje Genesis Ltd (Namungo) amesema mgodi huo umezalisha ajira za moja kwa moja 4,678 na ajira zisizo rasmi 3,250, hivyo kufikisha jumla ya ajira 7,928 kwa Watanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!