Latest Posts

CHAUMMA ZIARANI KIGOMA, YASEMA ITADAI HAKI NA KATIBA MPYA KWA MARIDHIANO

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Benson Kigaila kimesema kitaendelea kudai haki na katiba mpya kwa kukaa kwenye mezani ya maridhiano.

Kigaila amesema hayo Julai 28, 2026 wilayani Uvinza mkoani Kigoma wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho ya Tujenge Pamoja Tanzania.

Ameeleza kuwa kupitia maridhiano kutakuwa na fursa kubwa kwa Watanzania kujadili na kutoa maoni kwa pamoja juu ya matatizo yao ambayo wanatamani kufanyiwa marekebisho kwenye katiba mpya, akisisitiza kuwa katiba ya mwaka 1977 imepitwa na wakati na haiwezi tena kubeba hali halisi ya maisha ya Watanzania wa sasa.

“Sisi CHAUMMA tutasema Katiba ya mwaka 1977 haifai tena leo kwa sababu imepitwa na wakati. Ni sawa na suruali ya ‘Pepo’ ya miaka ya nyuma leo huwezi kuivaa! Tunahitaji Katiba mpya iliyoandikwa kwa maoni ya leo ya Watanzania, itakayoweka muafaka wa kitaifa na kumaliza migogoro ya ardhi, matatizo ya kisiasa na ukosefu wa ajira kwa vijana,” amesema Kigaila.

Ziara hiyo mkoani Kigoma pia inahusisha kuimarisha miundombinu ya chama hicho mashinani pamoja na kukusanya maoni ya wanachama kuhusu marekebisho ya Katiba ya CHAUMMA.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!