Latest Posts

WAZIRI MKUU MPYA ABARIKI MAREKANI KUTUMIA VITUO VYA KIJESHI VYA UINGEREZA

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Andy Burnham, ameidhinisha Jeshi la Marekani kuendelea kutumia vituo vya kijeshi vya nchi hiyo kwa ajili ya operesheni za kijeshi dhidi ya Iran, huku Serikali yake ikisisitiza kuwa ruhusa hiyo ni kwa ajili ya usalama na ulinzi pekee.

 

Uamuzi huo unaiwezesha ndege za kivita za Marekani kuendelea kutumia kituo cha RAF Fairford kilichopo Gloucestershire, pamoja na kituo cha pamoja cha kijeshi cha Uingereza na Marekani cha Diego Garcia kilichopo Visiwa vya Chagos, bila kuhitaji mabadiliko ya sera za sasa za Uingereza.

 

Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu imebainisha kuwa ruhusa hiyo imewekewa mipaka thabiti, ikieleza kuwa operesheni hizo zinapaswa kulenga tu kulinda usafirishaji wa meli za kimataifa katika Njia ya Bahari ya Hormuz (Strait of Hormuz), na lazima zizingatie sheria za kimataifa pamoja na haki ya kujilinda.

 

Hatua hiyo, inayokuja siku chache tu tangu Burnham achukue mikoba ya uongozi wa nchi, imekuwa mtihani wake wa kwanza wa kidiplomasia na kisiasa, akijaribu kuweka urari kati ya ushirika wa kihistoria wa Uingereza na Marekani na masharti ya kisheria yanayohusu mgogoro unaoendelea kupanuka nchini Iran na Mashariki ya Kati.

 

Kabla ya uamuzi huo, kukiwa na vikao vilivyoongozwa na Sir Keir Starmer kabla ya kuondoka madarakani, maafisa wa ngazi ya juu wa usalama na mawaziri walipitia kwa kina maombi ya Washington ili kujiridhisha kama matumizi ya vituo hivyo yanakidhi masharti ya sheria za kimataifa.

 

Katika vikao hivyo, Uingereza ilikuwa tayari imekataa maombi ya Marekani ya kutumia ndege zake za kisasa za B-2 Stealth Bombers kurusha mashambulizi kutoka Diego Garcia, kwa hofu kuwa mashambulizi hayo yanaweza kukiuka sheria za kimataifa na kuvuka mipaka ya haki ya kujilinda.

 

Badala ya kuleta sera mpya, Burnham amechagua kuendeleza masharti yaliyowekwa na mrithi wake, Sir Keir Starmer. Hatua hii inalenga kuepusha mtafaruku mpya wa kidiplomasia kati ya London na Washington, kufuatia kutoridhishwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, mapema mwaka huu baada ya Uingereza kugoma kutoa fursa ya mashambulizi ya moja kwa moja kutoka Diego Garcia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!