Latest Posts

AFGHANISTAN YASAINI SHERIA TATA: VIPIGO KWA FAMILIA SASA NI ‘HALALI’ MRADI MIFUPA ISIVUNJIKE.

Kiongozi mkuu wa Taliban, Hibatullah Akhundzada, amesaini sheria mpya ya adhabu nchini Afghanistan ambayo inaruhusu wanaume kuwapiga wake na watoto wao, mradi tu vipigo hivyo havisababishi kuvunjika kwa mifupa au majeraha ya wazi mwilini.

Sheria hiyo ambayo imezua taharuki kimataifa, haikuishia hapo, bali imegawanya jamii katika madaraja ya kijamii, ambapo adhabu hutofautiana kulingana na hadhi ya mkosaji.

Kulingana na kituo cha habari cha FistPost, chini ya mfumo huu mpya, wasomi wa dini hupewa ushauri pekee wanapokosea, watu wa daraja la chini hukabiliwa na vifungo vya gerezani au adhabu za viboko.

Mazingira ya kisheria kwa wanawake yamezidi kuwa magumu, ambapo sasa mwanamke anaweza kufungwa hadi miezi mitatu gerezani ikiwa atatembelea ndugu zake bila ruhusa ya mumewe. Aidha, mwanamke anapodai kufanyiwa ukatili mahakamani, analazimika kuleta ushahidi akiwa amejifunika mwili mzima na akiwa ameambatana na mlezi wa kiume

Shirika la kutetea haki za binadamu la Rawadari limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia kati mara moja. Mtaalamu wa UN, Reem Alsalem, ameelezea sheria hiyo kama “ya kutisha” kwa wanawake na wasichana, akisema inahalalisha ukatili wa kijumbani na kuwanyima binadamu utu wao wa msingi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!