Latest Posts

AGIZO LA MAKAMU WA RAIS LATEKELEZWA WANGING’OMBEl

 


Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Zacharia Mwansasu ameagiza wananchi wilayani humo kupanda miti na kuitunza ili kuboresha hali ya hewa inayoonekana kuvurugwa na baadhi ya watu wasiokuwa na elimu ya utunzaji wa mazingira.

Mwansasu ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la upandaji wa miti uliokuwa ukifanyika katika shule ya sekondari Igwachanya uliongozwa na kamati ya maandalizi ya siku ya masitu Duniani kuelekea kilele cha siku hiyo unaotarajia kufanyika kitaifa March 21 mkoani Njombe.

“Tunapokosa mvua,mito ikikauka changamoto kubwa ni kwasababu uoto wa asili tumeuondoa na Wanging’ombe mwaka huu ni mashahidi ya kwamba pamoja na kwamba serikali ilitangaza tutakuwa na mvua za wastani lakini miaka yote tumekuwa na mvua ila mwaka huu zimepungua na baadhi ya wakulima wamepata changamoto ya mazao kuto kuwa vizuri”amesema Mwansasu

DC Mwansasu amesema swala la kupanda miti ni jambo la kwanza lakini swala la utunzaji ni jambo lingine hivyo halmashauri hiyo kwa maelekezo ya serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango imeendelea kupanda miti huku changamoto kubwa wanayokumbana nayo ikiwa ni utunzaji.

Emmanuel Msoffe ni Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii amepiga marufuku wananchi kuvuna miti michanga na badala yake kuendelea kuongeza thamani ya mazao ya misitu ili kukomboa jamii kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!