Latest Posts

AKILI MNEMBA KUTUMIKA KUTOA TAARIFA ZA TAHADHALI YA HALI MBAYA YA HEWA

 

Serikali imezindua mradi wa miaka mitatu wa utoaji taarifa za tahadhari kuhusu matukio ya hali mbaya ya Hewa huku ikisisita kuendelea kuelimisha jamii dhidi ya matukio hayo na kuwajengea uwezo wataalamu kuhusu matumizi ya TEHAMA katika kutoa taarifa ya tahadhali ya majanga hayo kwa kutumia akili Mnemba.

Uzinduzi huo wa Mradi unaotambulika kama ‘Early Warning for All’ ama kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa tahadhari za mapema kwa wote, umefanyika leo Jumatano Machi 19,2025 Jijini Dodoma.

Lengo la Mradi huo ni kupanua wigo wa Taarifa nakuweza kuwafikia Watu wote hususani wanaoishi Vijijini Kwakuwasaidia kuchukua tahadhari za mapema kabla ya kutokea kwa majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali mbaya ya hewa na tabia ya Nchi ili kuokoa maisha ya watanzania na mali zao.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya hali ya hewa Nchini TMA kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ikiwa ni mwitikio wa maelekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa ifikapo 2027 kila mtu anafikiwa na taarifa za tahadhari ya hali mbaya ya Hewa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!