Latest Posts

ALAB CONTRACTOR YAWANUFAISHA WAKAZI WA TARIME, YATOA AJIRA KWA JINSIA ZOTE

 

Na Helena Magabe-Tarime

ALAB CONTACTOR LTD ni Kampuni inayowanufaisha Wakazi wa Tarime kwa ajira za kudumu pamoja na ajira za muda mfupi,kwa sasa imeajiri Wanawake na Wanaume kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya lami unaoendelea katika Kata ya Bomani Tarime Mjini.

Katika mahojiano na Jambo TV Machi 28,2025 Mhandisi wa Kampuni ya ALAB CONTRACTOR LTD ,Laurent Mwita Manko alisema Kampuni hiyo imeajiri Wanawake kwa Wanaume ili kuwakwamua kiuchumi licha ya kuwa wamo wenye ajira za kudumu pamoja na ajira za muda mfupi ambapo mradi huo kwa sasa unatekelekwa katika barabara mbili ambazo ni barabara ya Soroneki pamoja na barabara ya Utawala Bomani.

Alisema mradi ulianza Novemba 6,2024 utakamilika Julai 18,2025 , jumla ya mita 890 zinatekelezwa ambapo bara bara ya Soroneki ina urefu wa mita 390 huku bara bara ya Utawala Bomani ikiwa urefu wa mita 500 na kuongeza kuwa utekelezaji umefikia asilimia 60 na ujenzi huo unaendelea vizuri kufatia uwepo vitendea kazi vya kutosha.

Alieleza juu ya hatua za utengenezaji wa barabara kuwa, ya kwanza ni kusafisha barabara kwa kutoa nyasi (road clearness),hatua ya pili ni kutoa udogo mbaya,hatua ya tatu ni kuchimba tabaka mbovu na kuweka pembeni harafu zinawekwa kwa kupangwa hatua hizo ziko nne G7,G15,G45 pamoja na C 2 ambayo inachanganywa na simenti harafu rami nyeusi kisha inafata kokoto na mwisho rami yenyewe.

Hata hivyo Manko alifafanua kuwa mradi huo unatekelezwa na
JOSSAM & COMANY LTD ndiye Mkandarasi mkubwa kwenye mradi huo na makao yake makuu ni Kahama, lakini waliukabidhi mradi huo kwa ALAB CONTACTOR LTD Mkandarasi mdogo ambaye makao yake makuu ni Tarime ikumbukwe kuwa kampuni hii ya ALAP ni kampuni ambayo imejitoshereza inajishughulisha na ujenzi wa barabara pamoja na shughuli za migodini.

” Mimi ni site Agent kwenye mradi huu kwenye kampuni ya ALAB ni Mhandisi lakini mradi huu sisi ni Sub Contractor Main Contractor ni Kampuni ya JOSSAM& COMPANY n ndiye mtekelezaji tuko kwenye hatua nzuri maana vifaa tunavyo vya kutosha mradi unaendelea vizuri” alisema Manko

Kwa upande wake Bi Paula Charles Masawe amesema kampuni hiyo haina ubaguzi wa ajira inajali wafanyakazi wake na inatoa mshahara mzuri na kwa wakati hivyo ameshauri kina mama kujiunga kwenye kampuni hiyo ili wapate kipato kwaajili ya Familia zao kwani yeye ananufaika kwa mahitaji mbali mbali yakiwemo mahitaji ya watoto wa shule.

Naye Abakhari Ramadan Said ambaye ana miezi mitatu katika kampuni hiyo alisema hajaona changamoto yoyote katika ambapo amewashauri vijana wasiotaka kujishughulisha na kazi yoyote na kujihusisha na mambo yasiyo na maana waachane na tabia hizo watafute kazi kwenye kampuni ya ALAB.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!