Ili kupata matokeo mazuri katika utendaji kazi , moja ya mambo muhimu ya kuzingatia ni sharti kuwepo kwa mazingUjsira mazuri ya utendaji kazi kwa watumishi.
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amelithibisha hilo wakati wa ziara yake akikagua ujenzi wa ofisi za taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Maji.
Amekagua eneo unapofanyika ujenzi wa ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Maji, na ofisi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma pamoja na kituo cha ubora kinachosimamiwa na idara ya rasilimali za maji.
Mhe Aweso katika ukaguzi huo amemshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa Wizara ya Maji rasilimali fedha ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake.
Amezipongeza taasisi zote kwa hatua walizo fikia katika ujenzi na ameelekeza kuweka jitihafa zaidi ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati ili kuongeza ari kwa watumishi kutimiza azma ya serikali ya kufikisha huduma ya majisafi kwa wananchi kwa wakati kama ilivyopangwa.