Latest Posts

BARAZA LA WAFANYAKAZI TEA LAKUTANA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

 

Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) limekutana leo, Machi 10, 2025, mkoani Morogoro kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa majukumu ya idara na vitengo mbalimbali. Lengo ni kutathmini mwenendo wa mamlaka katika kufanikisha malengo yake na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho ili kuongeza ufanisi.

Katika kikao hicho, wajumbe walichambua changamoto zilizopo na fursa za kuboresha utendaji wa TEA, pamoja na kujadili mikakati ya kuimarisha mchango wa mamlaka katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini. Pia, wamesisitiza matumizi bora ya rasilimali na ushirikiano wa ndani kwa maendeleo ya sekta ya elimu.

Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya idara na vitengo mbalimbali ili kufanikisha majukumu ya mamlaka. Amehimiza wafanyakazi kuwa tayari kutekeleza majukumu yoyote yatakayoelekezwa kwa mafanikio ya taasisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!