Latest Posts

BMH YAONDOA UVIMBE WA UBONGO UKUBWA WA PARACHICHI

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanikiwa kundoa uvimbe mkubwa wa ubongo kwa mwanamke wa umri wa miaka 32 mkazi wa Mtumba, jijini Dodoma.

Daktari Bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu, Maxgama Ndosi, aliyeongoza upasuaji huo, amesema jijini Dodoma leo kuwa uvimbe uliokuwa upande wa kulia wa ubongo wa mgonjwa ulikuwa na ukubwa wa tunda la parachichi.

“Alikuja akiwa hawezi kutembea baada ya uchunguzi wa kitabibu tukagundua ana uvimbe mkubwa kwenye ubungo ambao ulihitaji upasuaji wa haraka ili kumuokoa,” amesema Daktari Bingwa wa Upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Bi Olivier Udoba, ambaye ni mama mzazi wa mgonjwa huyo, ameishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa huduma hiyo ya matibabu.

“Nawashukuru madaktari wa Benjamin Mkapa kwa huduma nzuri na kumuokoa mwanangu,” ameongeza.

Bi Udoba amefahamisha kuwa binti yake alianza kuumwa toka mwaka jana mwezi wa Septemba na kwamba alikuwa akipata changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo kupata degedege.

“Mwanzoni tulikuwa tumepanga kumpeleka Dar es Salaam hivyo tulivyoona hali yake inazidi kuwa mbaya tukabadili maamuzi tumlete hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa,” amesema Bi Udoba.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!