Latest Posts

BOND ZA BILION 1.5 ZIMENUNULIWA DODOMA

Baadhi ya wakandarasi, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa serikali wamenunua bondi zenye thamani ya Shilingi bilioni 1.5 kwenye Samia infrastructure bond mapema Jumatatu Desemba 16, 2024 Jijini Dodoma.

Bond hii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya barabara zilizo chini ya wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) zimenunuliwa wakati wa semina ya mauzo ya hatifungani ya Samia Infrastructure bond iliyoratibiwa na Bank ya CRDB

Akiongoza tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi huo na mikoa ya jirani kutumia fursa ya hatifungani ya miundombinu ya Samia kwa kujenga barabara imara na zitakazokamilika kwa wakati ili kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

”Wananchi wenzangu wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani tuitumie fursa hii kushirikiana na Watanzania wenzetu kujenga barabara imara, nazitakazokamilika kwa wakati ili tupite sisi, tusafirishe mazao yetu, nakusambaza bidhaa na huduma zitakazodharishwa kwaajili ya kila mmoja wetu, niwakaribishe wakulima kuweza kununua bondi hizi, nawakaribishe wakandarasi, wafanyabiashara, watumishi, taasisi za serikali ambazo malengo yake ni ya kufanya biashara,”

Aidha, Senyamule amesema elimu ya fedha kwa Watanzania wengi bado ni changamoto na kuendelea kuwasisitiza TARURA na CRDB kazi ya kuelimisha jamii kuhusu ununuzi wa bondi hisa iendelee kwa kasi kubwa ili kuhakikisha watanzania wengi wanatumia fursa hii kufaidika, na Samia infrastructure bond   na kushiriki kuchangia miundombinu ya nchi yao.

Naye Meneja TARURA mkoa wa Dodoma Mhandisi Edward Lemelo amesema “Sisi kama TARURA tumefarijika   na jambo hili kwa sababu changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi yetu ni kuchelewesha kuwalipa wakandarasi kwa hiyo tunaamini jambo hili litasaidia kulipa madeni yao kwa wakati, ”

Hatifungani ya miundombinu ya samia ni hati fungani mahsusi inayotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na miradi hii itaongeza mtandao wa usafiri nchini, ikiboresha kwa kiasi kikubwa usafiri wa vijijini na mijini na bondi hii inalenga kukusanya bilioni mia hamsini (150,000,000,000/=) na imepitiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CMSA.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!