Latest Posts

BOTI YAZAMA ZIWA VICTORIA, WATU SABA WAHOFIWA KUFARIKI KALANGALA, UGANDA

Takriban watu saba wanahofiwa kufariki dunia nchini Uganda baada ya boti ya mizigo kupinduka katika Ziwa Victoria alfajiri ya Jumatatu, ikiwa safarini kutoka kisiwa cha Kalangala kuelekea jiji la Entebbe. Boti hiyo, ambayo ilikuwa imebeba magunia ya mkaa, ilikumbwa na upepo mkali na mawimbi mazito kabla ya kupinduka.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:00 asubuhi. Mashua ya wavuvi wa eneo hilo iliwaokoa watu watano waliokuwa wakielea juu ya magunia ya mkaa.

Mmoja wa walionusurika, Moses Bukenya, alieleza kuwa walikuwa jumla ya watu kumi na wawili katika boti hiyo. “Coxswain alituhimiza kurusha mizigo majini baada ya maji kuanza kujaa, lakini haikusaidia. Mashua ilipinduka na tukaanza kuogelea huku tukijishikilia kwenye magunia ya mkaa,” alisema Bukenya katika mahojiano na Gazeti la New Vision.

Kwa mujibu wa BBC, ajali hiyo imeongeza hofu juu ya usalama wa usafiri wa majini nchini Uganda, hasa katika Ziwa Victoria. Mnamo mwaka 2023, watu zaidi ya 20 walifariki dunia baada ya boti ya abiria iliyokuwa imejaa kupita kiasi kupinduka. Kadhalika, mwezi Novemba 2018, ajali nyingine kubwa ilisababisha vifo vya watu 30.

Wito umetolewa kwa mamlaka za usalama wa usafiri majini kuchukua hatua za dharura kuweka viwango madhubuti vya usalama, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kujiokoa (life jackets), ukaguzi wa mizigo, na elimu kwa wasafiri kuhusu tahadhari za dharura.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!