Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimetoa Sadaka ya Eid na Pasaka katika vituo vitano vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum na wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwawezesha kusherehekea vyema sikukukuu hizo.
Miongozi mwa Sadaka hizo ni Mchele kilo 500, Mbuzi wa tano, Mifuko mitano ya ngano, Juice pamoja na maji.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jumapili Machi 30,2025 Mara baada ya kukabidhi bidhaa hizo Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga amesema Chama hicho kimeo vyema kumuunga mkono Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa misaada kwa Makundi mbalimbali.