Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Temeke wamefanya Ziara ya kutembelea CCM Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Kwa lengo la kujitunza historia mbalimbali za harakati za Uongozi wa tangu Chama cha TANU hadi CCM ikiwamo eneo ambalo Muasisi wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere alifikia akianza mchakato wa kupata Uhuru wa nchi hii.
Viongozi hao wa CCM Temeke wamefanya Ziara hiyo ya siku moja ikiwa na lengo la kuadhimisha kumbukumbu ya Miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM ili kujifunza hatua mbalimbali Waasisi wa CCM walizopitia ikiwa ni pamoja na kuombewa ikiwa ni harakati za ukombozi wa taifa hili kutoka katika utumwa wa wakoloni.
Katibu wa vyuo Wanafunzi wa vyuo vikuu Dua Mkoga ambaye ni kiongozi wa CCM Temeke akizungumza Mara baada ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo Wilaya ya Bagamoyo amesema wameanua kwenda Wilaya ya Bagamoyo kwakuwa ni sehemu za kihistoria ambayo wamefika kujifunza waasisi wa TANU na CCM walikoanzia harakati zao za ukombozi ili kuendelea kukifanya CCM kuwa Bora zaidi katika utendaji kazi wao hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Dua pia amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa anayoendelea kuyafanya nchini kwa kutuletea maendeleo ambayo yanaendeleza maono ya waasisi wa taifa hili.
Kwa upande wake Katibu wa Siasa na uenezi kata ya Temeke Innocent Mahendeka ametaja maeneo mbalimbali waliyofanikiwa kutembelea kuwa ni pamoja na ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo, shina la CCM lililoanzia tangu Chama cha TANU maalufu kwa jina la Mti pesa, jengo la Ikulu ya Kwanza ya Africa Mashariki.
Maeneo mengine aliyotaja ni pamoja na Maeneo ya kihistoria ya machiefu kwenye magofu ya kale ya Kaole, Eneo la mnara wa TANU ambapo Nyerere alikutana na Shehk Ramiya, Mji mkongwe ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii wilayani humo.
Amesema wamejifunza Vitu vingi ambapo pia wameshuhudia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa Katika awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia.
Mzee Mwinyi Akida akizungumzia historia ya eneo ambalo Baba wa taifa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere amesema mwaka 1954 alikuja Bagamoyo na alikutana na wazee wa Bagamoyo Ili kuweza kuwapa taarifa za harakati za kupambania ukombozi wa nchi yetu wakati huo ikiitwa Tanganyika.
Mzee Akida alisema Mwalimu Nyerere akiwa Bagamoyo alikutana na Shehe Lamia ambaye alimshauri wafanye dua maalumu wakiwa wamefunga kwa siku moja ambapo Nyerere alikubali kufunga kwani lengo la Dua hiyo ilikuwa ni mwenyezi Mungu amfanikishe malengo yake ya kutuletea Uhuru wa nchi yetu.
“Baada ya kufanya Dua hiyo Nyerere aliendelea na safari zake za harakati za kupambania uhuru wa nchi yetu ambapo aliendelea kufanya mikutano mbalimbali akielezea azima yake” alisema Mzee Akida.
Naye Katibu wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Azimio wilayani Temeke Victoria Charles amesema ujio wao wilayani Bagamoyo wakitokea Temeke ni iumuenzi Rais Dkt Samia kwa aliyofanya kupitia CCM ambapo pia wamejifunza kuhusu Chama cha TANU hadi kupatikana CCM .
Aliongeza kuwa ziara hiyo imewapa picha kamili ya namna Mwalimu Nyerere alifanya katika Uongozi wake na aliahidi kuwaelezea Wana CCM wenzao na makundi mengine umuhimu wa kufika wilayani Bagamoyo ambako kuna historia mbalimbali za kuanza kwa harakati mbalimbali za maendeleo ya nchi yetu.