Latest Posts

CHANJO MPYA YA SINDANO YA KILA MWAKA DHIDI YA VVU YAKAMILISHA JARIBIO LA AWALI

Watafiti wamekamilisha jaribio muhimu la awali la usalama kwa chanjo ya sindano ya kila mwaka inayolenga kumkinga binadamu dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU). Matokeo ya jaribio hilo yameripotiwa katika jarida la matibabu la The Lancet kwa mujibu wa kituo cha habari cha BBC.

Chanjo hiyo, inayofahamika kama Lenacapavir, hufanya kazi kwa kuzuia virusi visiongezeke ndani ya seli, hivyo kupunguza uwezekano wa maambukizi.

Iwapo majaribio yajayo yatafanikiwa, chanjo hii itakuwa hatua muhimu katika kuleta njia ya muda mrefu zaidi ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa sasa.

Kwa sasa, watu wanaotumia kinga dhidi ya maambukizi ya VVU (PrEP) humeza tembe kila siku au kudungwa sindano kila baada ya wiki nne. Ufanisi wa Lenacapavir utatoa mbadala wa kudungwa sindano mara moja kwa mwaka, hatua inayoweza kurahisisha zaidi kinga dhidi ya VVU.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!