Latest Posts

CIA YAKANUSHA RIPOTI YA KIJASUSI ILIYOMKASIRISHA TRUMP

Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Ratcliffe, amesema mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran “yaliharibu vibaya” maeneo hayo na yamerudisha nyuma mpango wa nyuklia wa taifa hilo kwa miaka mingi.

Kauli hiyo imekuja kama mjibu wa ripoti ya kijasusi iliyovuja, ambayo ilipendekeza kuwa vituo muhimu vya Iran havikupata madhara makubwa, jambo lililoibua hasira kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye alisisitiza kuwa uvamizi huo umeharibu kabisa miundombinu ya nyuklia ya Iran.

“Maeneo muhimu ya nyuklia ya Iran yameharibiwa vibaya sana. Hatusemi mpango wao umesambaratika moja kwa moja, lakini madhara yaliyotokea si ya kubeza. Uwezo wao umerudi nyuma kwa miaka kadhaa,” alisema Ratcliffe mbele ya waandishi wa habari.

Ripoti ya awali iliyovuja kutoka moja ya taasisi za kijasusi za Marekani ilieleza kuwa hakukuwa na ushahidi wa uharibifu mkubwa katika baadhi ya vituo vya nyuklia vya Iran, jambo lililoibua mjadala mkali nchini humo na nje ya mipaka.

Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Truth Social, aliita taarifa hizo kuwa “za uongo na za kusikitisha”, akivituhumu vyombo vya habari kama CNN na New York Times kwa “kushirikiana kudhalilisha mafanikio makubwa ya kijeshi.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!