

Na Helena Magabe Tarime
MKuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele jana Machi 14,2025 alizindua katiba ya umoja wa Wenyeviti wa Halmashauri ya Mji Tarime na kufanya harambee na kufanikisha kupatikana 8,000,000 keshi,3,300,000 na ahadi 4,700,000 ambapo aliwaomba wenyeviti hao kujiepusha kuwa sehemu ya migogoro ya ardhi.
Gowele ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki yeye mwenyewe alichangia 300,000,na kuwaailisha 2,000,000 za Mhe Michaeli Kembaki huku akihamasisha wadau kuchangia hadi hadi jumla 8,000,000 .
Aliwambia Wenyeviti hao wasitumie umoja huo kwa maslahi yao binafsi ya kutaka kuwa na watia nia wao badara yake watumie umoja huo kusuruhisha migogoro hasa miogogoro ya ardhi kwa Wananchi Kwani Mtaji wao na mradi wao ni Wananchi hivyo wajiepushe kuwa sehemu ya migogoro hasa ya ardhi.
Akijibu moja ya changamoto zilizosomwa kwenye risala na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mawasiliano Medrick Chacha Matiko (Chacha barozi) kuhusu ukosefu wa ofisi kwa Wenyeviti pamoja na vitendea kazi alisema kuwa ameshawasiliana na Mkurugezi wa Halmashauri ya Mji kuhusu kila mtaa kupata ofisi pamoja na kila kata pia ipate ofisi.
Kwa upande mwingine aliwaomba Wenyeviti kuwashauri Wananchi kuchukua tahadhari na mlipuko wa ugonjwa wa kuharisha ambapo amewataka Wote kwa pamoja kusimamia usafi na kukangua nyumba kwa nyumba kama kuna vyoo sambamba na hilo alitoa tahadhari ya viashiria vya ugonjwa wa Mpox kwa kuwataka wananchi kuepuka kusalimiana kwa kutumia mikono na kutumia vitakasa mikono.
Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime aliyewasili jana Tarime Hamza Adamu aliwaomba Wenyeviti kuwa walinzi wema wa amani waisaidie Serikali kwa kusuruhisha migogoro na sio kuwa wachochezi wa migogoro kwani baadhi ya maeneo Wenyeviti wamekuwa ni sehemu ya migogoro hususani migogoro ya aridhi.
Mwenyekiti wa umoja huo Mwita Meck alisema Wenyeviti wote mitaa 81 ya Halmaahauri ya Mji ni Wanachama wa Umoja huo aliahidi kutumia umoja wao kwa maslahi ya Wananchi na si vinginevyo aliwashukuru Wadau wote walio changia umoja huo pamoja na MKuu wa Wilaya Meja Edward Gowele kwa ushirikiano mzuri na Wenyeviti hao.
Katibu wa umoja huo Sabato Marwa alisema umoja huo hautakuwa wa kisiasa na hawako tayari kutumiwa na mtu yeyote kwani ni umoja uliopo kwa mujibu wa sheria hivyo hautakuwa umoja wa migogoro bali umoja wenye tija kwa Wananchi kwani Katiba yao ndiyo itakayo waongoza.
Hawa ni baadhi ya wadau waliochangia Mseti Wangwe 500,000, Said Chambiri 500,000, Mhe Esther Matiko,500,000,Chacha Soya 1,000,000,Peter Zacharia 500,000 Kibiba Machage 1,000,000 Christopher Kangonye 200,000,Mseti Heche 100,000,Nyambari Nyangwine 200,000, Rhobi Samwel 200,000Pamoja Mugini Jacob Mkurugenzi Mara online 100,000,pamoja na kitabu cha Wageni chenye thamani ya 35,000.