Latest Posts

DC GOWELE: MAOFISA MAZINGIRA WANASHIKA VINYESI VYA WATU

Na Helena Magabe – Tarime

Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kuhara unaoendelea mjini Tarime, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, amesema kuwa amechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika lakini bado kuna watu wanaendelea kuchafua mazingira, hali inayowafanya maafisa mazingira kushika vinyesi vya watu.

Akizungumza na Jambo TV, jana 20, 2025, ofisini kwake, Gowele alisema kuwa licha ya jitihada kubwa alizofanya kwa kushirikiana na Watendaji, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa mitaa ili kuweka mazingira safi, bado kuna watu wasiozingatia usafi.

“Mfano, kuna shimo pale limejaa mavi. Sasa hivi, wapo watu wanaokojoa kwenye chupa za maji na kuzitupa ovyo, wengine wanajisaidia haja kubwa kwenye mifuko Wafanyabiashara wanajisaidia wanafuga mavi kwwnye mabox Ukiwaangalia kwa nje, wanonekana watu safi tena wa maana kabisa, lakini wanawatesa maafisa mazingira ambao wanapokusanya taka, wanakutana na vinyesi,” alisema Gowele.

Alieleza kuwa, kutokana na hali hiyo, wamefunga baadhi ya sehemu za biashara pia amefunga dampo lililopo kwenye mteremko harafu karibu na mto kwani wakati wa nvua linatiririsha uchafu kuelekea mtoni .

Aidha, alisema baadhi ya Wafanyabiashara wamefungiwa kwa sababu hawana vyoo, licha ya kuwa wengine wana leseni za kuuza vinywaji baridi, lakini wamekuwa wakiuza pia pombe kali nao wamefungiwa maana hawana vyoo kwaajili ya wateja wao ,kuna Vijana Rebu wanauza vinywaji take away choo cha Rebu kinafungwa saa mbili lakini Wao wanaofanya biashara hadi saa nne wamefungiwa pia.

Ili kuhakikisha usafi unadumishwa, alisema ametoa agizo kwa wataalamu kupita nyumba kwa nyumba kukagua vyoo katika makazi binafsi, majengo ya serikali, na maeneo ya maegesho ili kubaini kama vyoo vinavuja ili warekebishe haraka mfano choo cha stendi alisikia tetesi kuwa kina vuja ameagiza kikaguliwe ,pia nyumbani kwake alisema wapite wakague.

“Usafi wa mwisho wa mwezi sasa nataka uwe wa kweli Tarehe 29, mimi pamoja na kamati yangu ya ulinzi na usalama tutashiriki usafi wa pamoja na Askari wote kisha tukimaliza ntazungumza nao na kuanzia sasa, kila kata itenge muda wa kufanya usafi kila wiki. Aidha, kesho tutaendesha zoezi la upandaji miti Wenyeviti wote watafanya kazi hiyo na Mimi nitapanda miti eneo la nyumbani kwangu zoezi litaanza saa moja hadi saa 3 ” alisema Gowele.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!