Latest Posts

DC KASILDA ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE UTAKAO ZINDULIWA NA RAIS SAMIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Machi 09, 2025 anatarajiwa kuzindua rasmi mradi wa waji Same-Mwanga-Korogwe uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 300 ambao ni hatua muhimu katika juhudi za serikali kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watanzania, hususan katika maeneo ya Same, Mwanga na Korogwe.

Akitembelea mradi huo unaotekelezwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Tanga,Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni akiongozana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo amesema kuwa mradi huo ni muhimu kwani utachochea maendeleo kwa Wananchi wa Wilaya hiyo.

“Kupitia mradi huu, changamoto za upatikanaji wa maji katika maeneo husika zitapungua kwa kiasi kikubwa, hivyo kusaidia kuboresha hali ya maisha ya wananchi, sekta ya kilimo, mifugo, na viwanda vidogo vidogo” DC Mgeni

Ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maji kama sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma za msingi kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Same (SAMWASA), Mhandisi Rashidi Mwinjuma, alieleza kuwa mradi huu umefikia hatua nzuri ya utekelezaji na unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe.

Mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe unalenga kuhudumia zaidi ya wakazi milioni moja, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za maji safi na usafi wa mazingira.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!