Latest Posts

DC KISSA: CHANGAMOTO ZISIFANYE MUACHE KUPANDA MITI

Wanawake wametakiwa kuondokana na dhana kwamba uwekezaji katika sekta ya misitu haulipi kwa madai kuwa miti huchukua muda mrefu kabla ya kuvunwa pamoja na kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuungua kwa misitu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Kissa Kasongwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka kwenye mkutano wa Jukwaa la Wanawake katika Sekta ya Misitu 2026 lililofanyika mjini Makambako mkoani Njombe, kwa ufadhili wa mradi wa FORLAND.

Kasongwa amesema kuwa changamoto ya kuchelewa kuvuna miti haipaswi kuwakatisha tamaa wanawake, akisisitiza kuwa “miti ni pesa” na uwekezaji wake una faida ya muda mrefu.

Awali,mratibu wa mradi wa FORLAND kitaifa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Emma Nzunda, amesema kwa sasa wanawake wameanza kujihusisha zaidi na shughuli za misitu zikiwemo upandaji,uvunaji na biashara ya mazao ya misitu licha ya changamoto mbalimbali zinazoendelea kuwapo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Dk. Siima Bakengesa, ameeleza kuwa takribani hekta 48,000 za misitu nchini, sawa na asilimia 50, zinachangia mapato ya taifa pamoja na kipato cha mtu mmoja mmoja, wakiwemo wanawake waliopo kwenye sekta hiyo.

Kwa upande wao, baadhi ya wanawake wanaojishughulisha na biashara ya mazao ya misitu, akiwemo Joyce Mpogole, wamesema sekta hiyo ina fursa nyingi zinazopaswa kuchangamkiwa, licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa zikiwemo za kikodi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!