Latest Posts

DC MPOGOLO AVUTIWA NA KAZI ZA TEA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Edward Mpogolo, ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Maonesho ya Kitaifa ya Kazi za Utamaduni na Sanaa yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Maonesho haya yameanza rasmi leo, Aprili 24, 2025, yakikusanya taasisi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji wa utamaduni, sanaa na elimu.

Akiwa katika banda la TEA Bw. Mpogolo alipata fursa ya kujionea shughuli zinazotekelezwa na TEA, hususan miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini kupitia ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, maabara za sayansi, nyumba za walimu, mabweni na majengo ya utawala.

Aidha, Mpogolo alipata taarifa kuhusu utekelezaji wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), ambao umewawezesha zaidi ya Watanzania 49,000 kupata mafunzo ya stadi mbalimbali za kazi, na hivyo kuchangia katika kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

Bw. Mpogolo aliipongeza TEA kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha elimu na kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia elimu na mafunzo ya ujuzi, akisisitiza umuhimu wa taasisi hiyo kuendelea kufikia wananchi wengi zaidi kwa huduma zake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!