Ni siku ya tano ya Wiki ya Wateja Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile akiwa mgeni rasmi amehitimisha kilele cha wiki hiyo
Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini Tanesco kwa kujitoa kwao usiku na mchana kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa ya kusambaza umeme mjini na Vijijini
Aidha ametumia wasaa huo kutoa vyeti vya pongezi kwa Watumishi ambao wameongoza kutoa huduma kwa wateja na vyeti vya kutambua mchango wao kwa wateja wakubwa
Awali Kaimu Meneja wa Tanesco Ruvuma Mhandisi Boniface Malibe alisema kuwa ndani ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Shirika hilo limetoa elimu kwa wateja, kuwatembelea huko mtaani na kuwapa huduma
Mhandisi Malibe alisema kuwa Shirika la Tanesco linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika Vijiji, Vitongoji na mitaa kama adhima ya Serikali ilivyoweka.