Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamsaka dereva wa pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama bajaji aliyesababisha ajali maeneo ya kichangani Manispaa ya Morogoro
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi inasema tukio hilo limetokea Aprili 3.2025 asubuhi na kusababisha majeruhi kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa Fidelis Mauki mwenye umri wa miaka 68 mkazi wa Area Six wa kanisa la Katoliki Morogoro shirika la dini la ndugu wadogo Afrika.
Inasema majeruhi huyo alikimbizwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro lakini wakati akiendelea na matibabu majeruhi huyo alipoteza maisha.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva asiyefahamika jina wala anuani akiwa na bajaji isiyofahamika usajili kuendesha kwa uzembe na kumgonga mtembea kwa miguu na kutokomea pasipojulikana,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwaajili ya taratibu za kuwapatia ndugu.