Profesa Ezekiel Amri amesema matumizi ya Akili Mnemba hayaepukiki katika nyakati hizi za mabadiliko makubwa ya teknolojia ili kuakisi sera ya Taifa ya Mabadiliko ya Tehama.
Profes Amri ambaye ni Naibu Mkuu wa Taaisisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu amehimiza kwamba maboresho ya mitaala lazima yaendane na mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kwa kuzingatia vifaa vinavyotakiwa katika mafunzo, waalimu wenye weledi wa hali ya juu ili kuzalisha wahitimu wanakidhi soko la ajira.
Prof. Amri ameeleza hayo katika Warsha ya kujadili matokeo ya upimaji na udhibiti ubora wa Wanafunzi wanaotoka vyuoni na kwenda maeneo ya kazi ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikifanya maboresho ya mara kwa mara kwenye mitaala yake ili kukidhi mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuwaanda wahitimu wenye weledi unaoakisi uhalisi wa soko la Ajira.
“Vigezo vya kimataifa vinaakisiwa kwenye mabadiliko ya sayansi na teknolojia, Taasisi yetu (DIT) haiko nyuma, iko mbele zaidi kufuatilia mabadiliko yote yanayoendelea katika sayansi na teknolojia”
“Kwahiyo sisi vijana wetu tunawafundisha kwa kufuata mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kuboresha mitaala yetu kuhusiana na vifaa vinavyohitajika katika mafunzo na Walimu wanaohitajika kwa weledi wa hali ya juu” amefafanua Prof. Amri.
Kwa upande wake Mratibu hiyo Dkt. Upimaji na udhibiti ubora wa wanafunzi Dkt. Ambene Mtafya amesema warsha hiyo inayowakutanisha wadau wa Elimu, waajiri, wahitimu na mamlaka za udhibiti ina umuhimu mkubwa katika kutoa mrejesho wa ujuzi wa wahitimu maeneo ya kazi na kutoa fursa ya kufanya mijadala ya pamoja katika kuboresha mitaala iliyopo.
Dkt. Ambene ameongeza kuwa lengo la warsha hiyo ni kupokea maoni ya wadau waajiri ni wahitimu wenye weledi na ujuzi gani wanahitaji katika maeneo yao.
“Lengo ni kuhakikisha kwamba kinachotakiwa Sokoni ndicho ambacho unawajengea vijana kwasababu hamna mwajiri anayependa kuanza tena kuwafundisha waajiriwa.
Tunatamani mwajiri akimpata mhitimu aanze kumtumia na tunakuwa na warsha kama hizi ili kuhakikisha kwamba kama kuna mahali pana makosa yanarekebishwa katika mitaala, katika ufundishaji, katika mbinu zote zinazotakiwa na katika vifaa” Ameeleza Dkt. Ambene.