Latest Posts

DKT. EMMANUEL SHINDIKA ATEMBELEA BANDA LA TEA KATIKA HAFLA YA KUFUNGA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA

 

Mkurugenzi wa Elimu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Emmanuel Selemani Shindika ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo Oktoba 11, 2024, wakati wa hafla ya kufunga Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayofanyika katika viwanja vya Chipukizi, Tabora.

Dkt. Shindika alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko, katika hafla hiyo.

Akiwa katika banda la TEA, alipatiwa maelezo ya kina kuhusu jinsi TEA, kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), inavyotoa elimu ya ujuzi ambayo inanufaisha vijana na wanawake.

Juma la Elimu ya Watu Wazima lilifanyika kuanzia Oktoba 7 hadi 11, 2024, likiwa na kaulimbiu: “Ujumuishi katika Elimu Bila Ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!