Latest Posts

DKT. MOLLEL AWAONYA WATAALAMU WA TIBA ASILI KUTUMIA VIUNGO VYA BINADAMU NA WANYAMA

DKT. MOLLEL AWAONYA WATAALAMU WA TIBA ASILI KUTUMIA VIUNGO VYA BINADAMU NA WANYAMA

Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania Dk. Godwin Mollel, amewataka wataalamu wa tiba asili nchini kuacha matumizi ya viungo vya binadamu na wanyama katika huduma zao, akisisitiza kuwa dhana potofu zinazohusisha ngozi ya nyati, simba, na mkia wa nyumbu zinapaswa kukemewa vikali.

Dk. Mollel alitoa wito huo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili Kitaifa jijini Mwanza, Agosti 31, 2024, yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya kupitia Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

“Tunahitaji kuondokana na imani hizi potofu ili kunusuru maisha ya wanyama pamoja na binadamu. Hakuna sababu ya kuendeleza matumizi haya ya viungo vya wanyama kwa kuwa ni hatari kwa mazingira na ustawi wa binadamu. Sisi sote tunapaswa kukemea vitendo hivi, kulinda mazingira, na kuhakikisha tunawafichua wenye vitendo viovu,” alisema Dk. Mollel.

Aidha, ameitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya tafiti za kina kuhusu wataalamu wa tiba asili. NIMR inapaswa kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya dawa zinazotumika, kuhakikisha zinatunzwa vizuri, na kuendelea kuzalishwa kwa wingi.

Kwa upande mwingine, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Ahmad Makuwani, alikiri kuwa dawa zinazozalishwa na wataalamu wa tiba asili zimefanya maendeleo makubwa, huku mataifa mengine kama Angola yakizisajili kama dawa rasmi kwa matumizi ya binadamu.

Kilele cha maadhimisho hayo kilikutanisha waganga wa jadi na wataalamu wa tiba asili, kikiwa na lengo la kuboresha huduma za tiba asili na kutetea haki za wanyama katika utendaji wa tiba hizo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!