Latest Posts

DKT. NANAUKA: “ACHENI KUMEZA HABARI HASI”; AWASHAURI VIJANA TABORA KULINDA NDOTO ZAO DHIDI YA KELELE ZA JAMII.

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana Joel Arthur Nanauka amesisitiza Vijana wa Kitanzania kujiepusha na taarifa hasi katika maisha yao kwa kuchagua na kuchuja kile ambacho kijana anachokisikiliza, akisema katika maisha zaidi ya asilimia 85 ya taarifa wanazozipata Vijana wa Kitanzania zimekuwa taarifa hasi.

Akizungumza kwenye Kongamano la Vijana Mkoani Tabora, Mhe. Nanauka amesisitiza pia Vijana kuamini katika ndoto zao, akibainisha kuwa haiwezekani kuiona fursa ambayo huna ndoto nayo, na kwamba watu na maarifa ndiyo vitu pekee vinavyoweza kubadilisha watu kwenye maisha.

“Ukiwa na ndoto usikubali uchaguliwe step za kucheza na mtu mwingine, wewe ndio unajua ndoto yako, iamini ndoto yako na ipiganie ndoto yako. Asilimia 95 ya taarifa tunazozipata ni taarifa hasi katika jamii yetu na kati ya kazi kubwa tuliyonayo vijana ni kuchagua taarifa chanya, taarifa chanya zinatengeneza kesho yako.” Amesisitiza Waziri Nanauka.

Wizara ya Maendeleo ya Vijana iliyoanzishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mahususi kwaajili ya masuala ya Vijana imeendelea kuratibu na kusimamia programu mbalimbali za uwezeshaji wa vijana kiuchumi, kijamii na kitaaluma ikiwemo utoaji wa mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana, mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kuimarisha ushiriki wa vijana katika shughuli za uzalishaji mali pamoja na kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kupanua wigo wa fursa kwa Vijana ikijumuisha ajira, ubunifu, teknolojia na maendeleo ya stadi za kazi kulingana na mahitaji ya soko la ajira la sasa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!