Kamati ya Utendaji ya Dar es Salaam Staff Sports League (DSSL) imetangaza kuanza mchakato wa kutumia mfumo mpya wa usajili na uhakiki wa wachezaji wenye lengo la kuzuia watu wasio na sifa kushiriki mashindano hayo.
Akizungumza katika sherehe za kuhitimisha mashindano ya ligi hiyo Mwenyekiti wa BW. Japhari Mtoro alisema “Mashindano ya wafanyakazi lazima yalindwe kwa nguvu na wivu mkubwa, hivyo ni muhimu kuwekeza katika mifumo itakayozuia mtu yeyote asiye na sifa kushiriki mashindano hayo.
Akifafanua zaidi Mwenyekiti amesema kuanzia msimu unaokuja wataweka mfumo wa biometric utakaotumika kuwasajili na kuwatambua wachezaji kwa sura zao na alama za vidole.
Mashindano ya DSSL yanatajwa kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha afya, mahusiano na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi katika Jiji la Dar es Salaam.