Latest Posts

EDWIN SOKO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA MISA-TAN

Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) umefungua ukurasa mpya baada ya wajumbe kumchagua Edwin Soko kuwa Mwenyekiti wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Soko anachukua nafasi ya Salome Kitomari, ambaye ameiongoza MISA-TAN kwa mafanikio kwa kipindi cha miaka minane, tangu mwaka 2018.

Uchaguzi huo, uliofanyika leo, Jumatano, Desemba 4, 2024, katika ukumbi wa UCSAF Jijini Dodoma, unaleta mabadiliko muhimu katika uongozi wa MISA-TAN. Soko anatarajiwa kuendeleza juhudi za kukuza uhuru wa vyombo vya habari na kulinda haki za wanahabari nchini Tanzania na katika kanda ya Kusini mwa Afrika.

Msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi, Ali Aboth, alimtangaza rasmi Edwin Soko kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa MISA-TAN baada ya kupata kura 33. Said Mmanga aliibuka wa pili kwa kura 9, akifuatiwa na Betty Masanja aliyepata kura 3 kati ya kura 46 zilizopigwa, ambapo kura moja iliharibika.

Uongozi mpya wa MISA-TAN unatarajiwa kuimarisha zaidi nafasi ya taasisi hiyo katika kutetea na kuendeleza uhuru wa habari.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!