Latest Posts

FBI: MVULANA ALIWAUA WAZAZI WAKE KUPANGA NJAMA YA KUMUUA RAIS TRUMP

Mwanafunzi wa shule ya sekondari kutoka jimbo la Wisconsin, Nikita Casap (17), ameshtakiwa kwa kuwaua wazazi wake kama sehemu ya mpango mkubwa wa kumuua Rais wa Marekani Donald Trump, kwa mujibu wa ripoti ya FBI.

Katika hati mpya ya upekuzi iliyotolewa na mahakama, imeelezwa kuwa Casap alimuua mama yake, Tatiana Casap (35) na baba yake wa kambo Donald Mayer (51) mnamo Februari 11, 2025. Miili yao ilipatikana nyumbani kwao baada ya kijana huyo kutoweka shuleni kwa zaidi ya wiki mbili.

Wachunguzi wanasema Casap alikuwa na mawasiliano na watu nchini Urusi kuhusu njama hiyo, huku akipanga kutorokea Ukraine baada ya utekelezaji wa mpango wake. Polisi walimkamata katika jimbo la Kansas akiwa na gari la marehemu Mayer, bastola ya Smith & Wesson, kadi za benki, vito vya thamani, sefu na kiasi cha dola 14,000 zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya Biblia.

Simu ya kijana huyo ilikutwa na nyaraka zenye maudhui ya chuki dhidi ya Wayahudi, ushawishi wa kikundi cha Nazi kinachojiita Order of Nine Angles, pamoja na nyimbo za Adolf Hitler na mipango ya mapinduzi ya kisiasa. FBI imesema mauaji hayo yalionekana kama juhudi za kijana huyo kupata njia za kifedha na uhuru wa kuendeleza mpango wake wa kumuua Rais Trump.

Kwa sasa Nikita Casap anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya daraja la kwanza na makosa mengine saba ya jinai likiwemo kuficha maiti, wizi na kupanga njama za kigaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!