Latest Posts

GARI ILIYOTAIFISHWA NA TRA YAKABIDHIWA VETA MARA

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Mara imekabidhi gari aina ya Mitsubish Fuso katika chuo cha ufundi stadi Veta mkoani Mara liloingizwa nchini bila kufuata taratibu za kiforodha katika mpaka wa sirari wilayani tarime Mkoani Mara.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo meneja wa TRA mkoa wa Mara Nasoro Ndemo alisema gari hilo lilikamatwa katika oparesheni za kila siku zinazofanywa na kikosi cha kuzuia magendo mkoani Mara.

Nasoro amesema kamwe hakuna atakayepona ambaye hata faata sheria katika kuuingiza bidhaa kwanjia zisizo halali katika mpaka huo kwani vyombo vya usalama vimejizatiti kukomesha vitendo hivyo.

“ Gari hili liliingia nchini bila kufuata utaratibu likakamatwa utaratibu gari ikikamatwa katika magendo chombo kinaweza kutaifichwa na kikagawiwa kwa taasisi za serikali au kuuzwa kwenye mnada kwahiyo ukijihusisha na ukabainika vya magendo vyote vitataifishwa achene kufanya biashara za magendo nihasara” Nasoro Ndemo.

Katika hatua nyingine Meneja amewapongeza baadhi ya wafanya biashara ambao wamekuwa waaminifu na wamekuwa msaada katika kuhakikisha serikali haiapati hasara katika uingizaji wa bidhaa

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!