Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) imesema majalada 524 yasiyohusiana na masuala ya jinai ikiwemo ya kutaka uhalali wa wazazi wa mtoto yamechunguzwa ndani ya kipindi cha miaka minne.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Machi 14,2025 Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai wa mamlaka hiyo, Fidelis Bugoye wakati wa kuelezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita na mwelekeo wa mamlaka hiyo.
Amesema kuna ongezeko la watu wanaotaka huduma za vinasaba kwenye mamlaka hiyo, hali inayotokana na uelewa wa huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo na uhitaji wa taarifa za uchunguzi wa vinasaba kwa ajili ya maamuzi mbalimbali.
Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo imepata wito wa kusaidia kutoa ushahidi wa kimahakama 6986 ambapomafanikio hayo yanatoka na utendaji kazi wa ushirikiano na watendaji wa Mamlaka husika katika kufikia lengo la utoaji huduma bora kwa jamii.
“kuhudhuria wito wa Mahakama 6,986 kutoka mahakama mbalimbali nchini kwa ajili ya
kutoa ushahidi wa kitaalamu. Utoaji wa ushahidi huo umechangia katika mnyororo wa Haki Jinai kwa kutoa/maamzihaki kwa mhusika na kwa wakati, hivyo kuchangiakuleta, amani na utulivu wa nchi.”
“Mamlaka ina jukumu kutoa Ushahidi wa Kitaalam baada ya uchunguzi wa kimaabara katika mahakama nchini. Jukumu hili linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sura 177 na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura 20. Hivyo, kisheria matokeo ya uchunguzi wa kimaabara unaofanywa na Mamlaka matokeo ya uchunguzi yanatambulika Mahakamani kwa masuala yote yanayohusu Jinai.” Amesema.
Pia ameeleza kuwa mlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kujenga,kukamilishana kuanza kutumia jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, eneo la Medeli jijini
Dodoma ambao ujenzi wa Jengo hilo umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 8.14.