Na Helena Magabe -Mara
‎Mkurugenzi Mkuu wa kampuni binafsi ya uwekezaji ya HAIPPA PLC na Makamu wa Rais chemba ya biashara Tanzania Boniphace Ndego amesema kuwa HAIPPA PLC itafikia malengo ya dira ya Taifa 2050 ndani ya miaka 10 kulingana na uzoefu wake Pamoja na utalamu wake katika uwekezaji.
‎Hayo ameyasema baada ya kuhojiwa kama mtalamu wa uwekezaji kuwa inawezekanaje kwa Watanzania wa hali ya chini kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 kwa kuifanya Tanzania ifikie hadhi ya uchumi wa pato la Taifa kwa Mtu mmoja kufikia million 18 kwa mwaka ama shilingi millioni 1.52 kwa mwezi ama shilingi 50,000 kwa siku kama alivyonukuliwa Waziri wa mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo Julai 17,2025 siku ya uzinduzi wa Dira ya Taifa.
‎Ndengo anasema inawezekana kabisa na wao HAIPPA PLC ambao ni sekta binafsi ya uwekezaji watayafikia malengo ya Dira hiyo ndani ya miaka 10 ijayo ,ambapo kwa Watanzania kwa ujumla alisema wakipewa elimu ya uwekezaji kupitia fursa mbali mbali walizonazo wakafikia kiwango hicho cha kipato kilichotajwa hata kama ni wananchi wa hali ya chini sana.
‎Anasema inawezekana kabisa kuzalisha hata milioni moja na nusu 1.5 kwa siku endapo Watanzania watapewa elimu na maarifa ya kutosha kuhusu uwekezaji kwani watafundishwa, kwani HAIPPA ina mfumo wa kuwahudumia Watu wote wenye simu za aina zote kubwa na ndogo pia elimu itatolewa kupitia miradi iliyopo HAIPPA kama vile smatika mradi uliozizinduliwa Julai,1,2025.
‎HAIPPA ni kampuni ya Umma inaokuza biashara,uwekezaji,masoko na mikopo ambayo inaelimisha Umma na kuhimiza mambo manne ambayo ni elimu ya uwekezaji,ushiriki wa Watanzania kwenye uwekezaji mkubwa ,ubunifu na ujenzi wa biashara Pamoja na fursa za soko la HAIPPA kwa wabunifu,wajasiriamali,wahitimu,Vijana wenye vipaji ,Taasisi Pamoja na wawekezaji wadogo .
‎Anaelekeza kuwa katika mikakati yake imejenga HAIPPA kuwa kampuni ya Umma ambayo bidhaa zake ni Hisa,soko,mitaji Pamoja na huduma za HAIPPA naili kufanikisha malengo yake manne ambayo ni kutafasiri fursa za biashara kwenye sekta mbalimbali kwa jicho la uwekezaji,kutafasiri sera za Nchi kwa jicho la uwekezaji,kutafasiri mwenendo wa uchumi wa Dunia kwa kwa jicho la uwekezaji Pamoja na kusaidia kuingiza fursa za teknolojia ,taaluma,utawala bora kwenye biashara zilizo imara ,bora na zenye ufanisi.
‎Makundi yanayolengwa na huduma za HAIPPA ni Wananchi wenye vipato vya chini waliojiajiri,walioajiriliwa ,Pamoja na wajasiriamali kwenye sekta zote za kiuchumi vilevile kuna programu maalumu kwaajili ya Watumishi waliojiandaa kustaafu ,Vijana na Wanawake ,Kinababa,Watu wenye ulemavu na Watoto ambapo kwa msaada wa kidijitali huduma za HAIPPA zinafika Mikoa yote Nchini kwa Mjini na Vijijini ,kwa sasa HAIPPA ina Familia ya Wawekezaji 550 ambapo ilianza na Familia ya Wawekezaji 8.
‎Uzuri ni kwamba Mwekezaji anaweza kupitia hatua tano za HAIPPA kujisajiri na kujiunga kulingana na atakavyohitaji ya kwanza ni kujisajiri kupitia Tovuti ya HAIPPA ,App ya HAIPPA unachagua akaunti ama kujisajiri kupitia*149*46*23# ambayo ni rahisi anaweza kujiunga Mtu yeyote hata mwenye simu ndogo na kuendelea kupata huduma sawa na mwenye simu kubwa.
‎Baada ya kujiunga inatolewa elimu ya awali,malipo ya uanachama ,kuanza kuwekeza Pamoja na kuendeleza uwekezaji wake kwa kuendela kujifunza ,na kwenye elimu ya uwekezaji kuna mada kuu tatu ,maana ya uwekezaji,maana ya kampuni za umma Pamoja  na nafasi ya ubunifu ambapo mada zote tatu zinachambua kupitia mada ndogo(subtopcs) 140 ambazo mwanafunzi wao akihitimu atakuwa ni mtu huru wa kiuchumi.
‎Kwa muktadha huo Ndengo anatoa fursa kwa Watanzania kujiunga HAIPPA na kujifunza namna bora ya uwekezaji kwa kutumia fursa walinazo ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa 2050 kwani anasisitiza kuwa Wananchi watapewa elimu ya maarifa ya uwekezaji hivyo anawashauri Watanzania wajifunze kupitia HAIPPA watajenewa uwezo mkubwa wa uwekezaji na watakuwa Wawekezaji wakubwa.