Uchunguzi mpya wa kura za maoni unaonesha Kamala Harris anaongoza dhidi ya Donald Trump huko Pennsylvania. Harris na Trump wanashindania kura muhimu 19 za Pennsylvania.
Wagombea hao wa urais wamekuwa wakifanya ziara za mara kwa mara katika jimbo hilo. Harris anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara Philadelphia usiku wa kuamkia Siku ya Uchaguzi.
Karibu tafiti zote za kura za maoni huko Pennsylvania zinaonyesha tofauti ndogo kati ya Harris na Trump. Kulingana na utafiti wa mwisho wa kabla ya uchaguzi wa Morning Call/Muhlenberg College uliowahusisha wapiga kura 460 walio na uwezekano mkubwa wa kupiga kura, utafiti huo uliofanyika kuanzia Oktoba 27 hadi 30 na kuchapishwa Jumapili, makamu wa rais ana uongozi wa alama mbili dhidi ya Trump, asilimia 49 dhidi ya 47.
Uongozi wa Harris uko ndani ya kiwango cha makosa ya takwimu cha asilimia 6, ambayo pia inaonesha ongezeko la alama moja ikilinganishwa na utafiti wa awali wa Morning Call/Muhlenberg College wa wapiga kura 450 wa jimbo hilo uliofanywa Septemba 16 hadi 19. Utafiti huo wa awali ulikuwa na asilimia sawa, na ulionesha Harris na Trump walifungana kwa asilimia 48.
Ingawa uchaguzi unaendelea kuwa na ushindani mkubwa, asilimia 2 ya walioshiriki katika utafiti wa Jumapili walieleza kuwa bado hawajamchagua mgombea. Waliohojiwa walisema kuwa bado “hawajaamua.”
Utafiti huu, kama ilivyo kwa tafiti nyingine, umeonesha mgawanyiko wa kijinsia na rangi. Umeonesha Harris anapendelewa na wanawake kwa asilimia 53 dhidi ya asilimia 43 ya Trump, wakati Trump anaongoza kwa wanaume kwa asilimia 52 dhidi ya asilimia 43 ya Harris. Wapiga kura wazungu wanamuunga mkono Trump kwa asilimia 54 dhidi ya asilimia 43 ya Harris, wakati wapiga kura wa jamii za watu wa rangi wanamuunga mkono Harris kwa asilimia 66 dhidi ya asilimia 27.
Kulingana na tafiti nyingine, jimbo hili linakabiliwa na ushindani mkali. Trump alikuwa akiongoza jimbo hilo kwa asilimia 0.3 kufikia Jumapili, kulingana na wastani wa tafiti tatu – 538, RealClearPolling, na Silver Bulletin ya Nate Silver. Kulingana na wastani wa tafiti za The Times, Trump anaongoza kwa asilimia 49 dhidi ya asilimia 48 ya Harris. The Hill’s wastani wa tafiti ulionyesha Trump ana uongozi wa alama 0.7, kwa asilimia 48.8 dhidi ya asilimia 48.1 ya Harris.