Latest Posts

HATIMAYE OBAMA AMUUNGA MKONO KAMALA HARRIS KUWA RAIS MAREKANI

Na Ritha Mushi.

Rais wa zamani Barack Obama amemuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic, na hivyo kumaliza uvumi kuhusu kutomuunga mkono.

Kwa mujibu wa BBC Swahili Obama na mkewe Michelle Obama wamesema katika taarifa ya pamoja kwamba wanaamini Harris ana maono, tabia, na uwezo ambao unahitajika katika kipindi hiki kigumu.

Pia Obama ameripotiwa kuwa miongoni mwa zaidi ya wanademokrasia 100 mashuhuri ambao Harris alizungumza nao baada ya Rais Joe Biden kutangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Kamala Harris tayari amepata uungwaji mkono wa wajumbe wengi wa chama chake, na hivyo kumweka katika nafasi nzuri ya kuteuliwa rasmi katika kongamano la chama hicho linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

“Tunakubaliana na Rais Biden,” ilisema taarifa ya wanandoa hao, “kumchagua Kamala ilikuwa mojawapo ya maamuzi bora aliyofanya. Huku wakiahidi kufanya kila wawezalo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!