Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mhandisi Fatma Rembo leo Januari 31 anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Fatma, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la UWT kutoka Mkoa wa Iringa, ameendelea kuwa nguzo muhimu katika harakati za kuwawezesha wanawake na kuhakikisha maendeleo ya jamii kupitia nafasi yake ndani ya jumuiya.
Katika siku hii muhimu, familia, marafiki, na wanachama wa UWT wanamtakia maisha marefu, afya njema, na mafanikio zaidi katika jitihada zake za kuwatumikia wanawake wa Tanzania.
Kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla, anasalia kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi wa sasa na wa baadaye.