Latest Posts

HUDUMA HOSPITALI YA MAWENZI ZAZIDI KUIMARIKA

Mbunge wa Moshi mjini Mhe. Priscus Tarimo amekabidhi gari moja la kubeba wagonjwa(ambulance) na kuzindua ukarabati wa wodi ya upasuaji kwa wanaume katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa katika kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma ya afya, serikali imekuwa ikitoa pesa nyingi kwa ajili ya maendeleo ya mkoa hasa katika jimbo la Moshi Mjini.


Ameongeza kuwa katika bajeti iliyopitishwa na bunge tayari serikali imetenga bilioni 2 kwa lengo la kujenga jengo la kitengo cha upasuaji ili kukabiliana na wingi wa wagonjwa wanaopatiwa rufaa kwenda hospitali ya kanda.

“Bado uhitaji ni mkubwa wa huduma ,wagonjwa ni wengi kuliko uhitaji ,hivyo kwenye bajeti ya mwaka huu serikali imetenga bajeti ya bilioni 2 kwenye bajeti ya mwaka huu,yaani tukianza huduma hizo tunaendelea kupunguza ongezeko la wagonjwa wanaopatiwa rufaa kwenda hospitali ya kcmc” Amesema Priscus.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi Edna-joy Munisi akielezea upanuzi wa huduma mbalimbali katika hospitali hiyo ,ameipongeza serikali kwa kuendelea kusogeza huduma bora za afya kwa wananchi.

“Tunatarajia hivi karibuni kuanza kutoa huduma za kusafisha figo katika hospitali yetu na jumla ya vitanda 10 pamoja na mashine zake tutaenda kutoa huduma hii kwa wakati mmoja” Amesema Munisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!