I.P.I WASIKITISHWA NA TUKIO LA NABII ALIYEWACHAPA VOBOKO WAUMINI KANISAN
Theophilida Felician.
Taasisi inayojishughulisha na utoaji elimu ya amani hapa nchini, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla INTERNATIONAL PEACE INFOMATION I.P.I imelaani tukio la mchungaji Kelvin nchini uganda aliyewachapa viboko kanisani kwake kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuwapa Baraka.
Akitoka kauli ya masikitiko juu ya tukio hilo Rais wa I.P.I akiwa na viongozi wenzake ofisi za makao makuu ya taasisi Temeke Dare es salaam Prof Wilson George Munguza amesema tukio hilo ni laudharirishaji na halikubaliki kamwe kwenye jamii.
Amefafanua kwamba baada ya kuona vyombo vya habari vikiripoti tukio hilo zikiwemo vidio zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii limewashangaza na kuwasikitisha kwani kufanya hivyo nisehemu ya viashiria vya uvunjifu wa amani.
Amesema kufuatia hilo tayari wameisha toa maelekezo kwa viongozi wa taasisi I.P.I kwa upande wa Uganda kushirikiana na serikali ya Uganda katika kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ili aweze kuchukuliwa hatua muchungaji huyo pengine kabla ya kusababisha madhara zaidi.
Kwa mjibu wa Prof Munguza amebainisha vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo kuwa waumini bila kuzingatia umri wao wazee kwa vijana na akina mama wamehusika kuchapwa viboko ili kuvuna Baraka za mwenyezi Mungu.
Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani hususani hapa nchini kuendelea kuwa makini ili viongozi wa dini kama Kelvin wasipate upenyo wakuendesha maovu yao kwa wananchi kama ilivyokwisha fanya kwa nabii mchawi kutoka Congo aliyefukuzwa baada ya kwenda kinyume na utaratibu.
Amehitimisha akisisitiza kuwa wao kama taasisi maeneo yote watashirikiana na serikali kufichua uhalifu wa aina yoyote unaoweza kusababisha uvunjifu wa amani.