Latest Posts

I.P.I WATUA UGANDA KUHAMASISHA AMANI

Na. Theophilida Felician.

Taasisi ya INTERNATIONAL PEACE INFORMATION I.P.I. inayojikita kutoa elimu kwa wananchi hapa nchini na Afrika mashariki imefika nchini uganda kwa ajili ya kuhamasisha elimu ya amani kwa waganda.

Ziara ya I.P.I ikiongozwa na Rais wake Prof Wilson George Munguza imeyatembelea maeneo kadhaa ikiwemo kufanya mkutano mkubwa wilaya ya Buwela mkoani Jinja.

Prof Munguza akihutubia katika mkutano huo awali ameipongeza serikali ya uganda inaongozwa na Yoweri Kaguta Museven kwa namna inavyodumisha amani inayopelekea wananchi na wageni kuishi kwa utulivu nchini humo.

“Ndugu zanguni waganda nchi bila ya amani hapakaliki mnakumbuka yaliyotukumba mwaka 1978_1979 vita ile ya Kagera baada ya aliyekuwa Rais wenu wakati huo Hayati Idd Amini kutuvamia amani ilitoweka kati yetu na nyinyi pia watanzania walipoteza maisha sambamba na waganda, huo mfano tuu hivyo sisi kama taasisi kuja na malengo haya yakuhamasisha amani tunatamani kuona inaendelea kudumishwa kama ilivyo kwa sasa” amesema Rais wa taasisi Prof Munguza.

Amepongeza umoja na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili Tanzania na Uganda akisema kwamba ni hatua nzuri ya kujenga umoja na mshikamano thabiti huku akiishukuru serikali ya uganda kwa ushirikiano wanaoutoa kwa taasisi hiyo katika utendaji kazi wake bila ya bughudha.

Hata hivyo amewapongeza waganda likiwemo jeshi la polisi la nchi hiyo kwa mapokezi mazuri waliyoyaonyesha kwao ambapo amewaahidi kuendelea kuwafikia na nchi nyingine katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kwingineko.

Naye Rais wa umoja wa amani kwanza nchini uganda Shantari Kaitesi amepongeza ugeni huo kutoka Tanzania na kufika Uganda kueneza injili ya amani.

Ameongeza kuwa wao kama waganda wamefarijika mno na ziara hiyo huku akiwapongeza viongozi wa serikali mbili Tanzania na uganda kwa kudumisha ujirani mwema na wananchi wanaungana na kuendesha shughuli zao zikiwemo za kibiashara bila misukosuko.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!