Latest Posts

I.P.I YAKEMEA KAULI ZA KICHOCHEZI DHIDI YA WANASIASA

Theophilida Felician.

Taasisi ya INTERNATIONAL PEACE INFOMATION I.P.I inayohusika na utoaji elimu ya kuitunza amani hapa nchini imekemea kauli na matamshi ambayo yana viashiria vya uvunjifu wa amani kama ambavyo imeanza kujitokeza.

Ametoa kauli hiyo Rais wa taasisi hiyo Prf Wilson George Munguza kwenye kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya wawakilishi kutoka vyombo vya ulinzi na usalama makoa makuu ya I.P.I yaliyopo Temeke Dare es Salaam.

Amefafanua kwamba kauli za namna hiyo hazipaswi kupewa nafasi hususani nyakati kama hizi ambazo taifa linaelekea kufanya tukio muhimu la uchaguzi mkuu wa viongozi, ambao ni madiwani, wambunge na Rais.

Ameeleza kwamba ni vyema kila wanasiasa na vyama vyao wakatumia busala katika kufanya shughuli za kisiasa badala ya kujikita kwenye mambo yasiyo rafiki kwa nchi kama ambavyo imeanza kujitokeza.

Amewasihi wananchi, viongozi wa dini na makundi mengine kusimama na kushikamana katika kuitunza amani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!