Latest Posts

JAMII YAOMBWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ZA MITAA

Jumla ya watoto 8,372 wanaoishi na kufanya kazi mtaani katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania waliokolewa kutoka mitaani kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025.

Akizungumza Leo Aprili 12,2025 katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto Anaeishi na Kufanya Kazi Mtaani Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Dkt.Doroth Gwajima amesema watoto wengi hukimbilia kuishi na kufanya kazi mtaani kutokana na kukosa ufumbuzi dhidi ya changamoto zinazowakabili.

Hivyo ameisisitiza jamii kutoa taarifa kwa wakati kuhusu changamoto za kifamilia ambazo ni tishio kwa ustawi wa watoto ili wataalamu wa ustawi wa jamii waweze kushirikiana na familia au jamii husika kwaajili ya kupata ufumbuzi.

 

Akizungumzia sababu kuu inayopelekea watoto kuingia mtaani ni pamoja na migogoro ya kifamilia,ukosefu wa usawa na hali duni ya maisha hivyo ameisisitiza jamii kushirikiana na serikali za mitaa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala mkoa utaendelea kuweka mikakati endelevu ya kukabiliana na changamoto ya watoto wa mitaani ikiwemo kutoa elimu kwa wazazi na walezi ili kuimarisha malezi bora na kulinda haki za watoto kwa mujibu wa sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!